MTANGAZAJI

MAAFA UPARENI TANZANIA

MVUA kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia jana wilayani Same, imeleta maafa makubwa baada ya watu wapatao 25 kuhofiwa kufa kufuatia kitongoji chao kufukiwa na kifusi cha mlima uliopromoka na kuzifunika kabisa nyumba zao usiku wa manene wakiwa usingizini.

Vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini jana na leo vimeeleza kuwa Tukio hilo limetokea wakati mvua ambayo imenyesha kwa siku tatu mfululizo katika kata za Maore, Ndungu, Kihurio, Bendera ikiwa imesababisha maafa makubwa na kusababisha vifo vya wanafunzi wawili ambao walisombwa na maji.

2 comments

viva afrika said...

ni msiba wa kitaifa, tusikome kumwomba mungu katika kipindi hiki.

Anonymous said...

We are praying...it is a terrible disaster indeed.

Mtazamo News . Powered by Blogger.