MTANGAZAJI

SERIKALI YA TANZANIA YATANGAZA RASMI MIKOA NA WILAYA MIPYA

SERIKALI YA TANZANIA YATANGAZA RASMI MIKOA MIPYA MINNE NA WILAYA 19

SERIKALI ya Tanzania  imetoa matangazo rasmi ya Serikali (Government Notices)
kuhusu uanzishaji wa mikoa mipya minne na wilaya mpya 19 ambayo
yamechapishwa tangu Machi 2, mwaka huu.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema matangazo hayo ambayo yalisainiwa na

Rais Jakaya Kikwete tangu Machi mosi, 2012, yanabainisha mikoa mipya
kuwa ni Geita, Katavi, Njombe na Simiyu. Mikoa hii imechapishwa katika
Tangazo la Serikali Na. 72.

Wilaya 19 ambazo zimeanzishwa na kuchapishwa katika Tangazo la

Serikali Na.73 ni Buhigwe, Busega, Butiama, Chemba, Gairo, Ikungi na
Itilima. Wilaya nyingine ni Kakonko, Kalambo, Kaliua, Kyerwa, Mbogwe,
Mkalama na Mlele. Nyingine ni Momba, Nyang’hwale, Nyasa, Uvinza na
Wanging’ombe.

Kwa mujibu wa matangazo hayo makao makuu ya mikoa hiyo mipya minne

yatakuwa kama ifuatavyo: Geita (Geita), Simiyu (Bariadi) Njombe
(Njombe) na Katavi (Mpanda).

Mikoa hiyo itakuwa na wilaya zifuatazo; Geita utakuwa na wilaya tano

za Bukombe, Chato, Geita, Mbongwe na Nyang’hwale. Mkoa wa Katavi
utakuwa na wilaya mbili za Mlele na Mpanda. Mkoa wa Njombe utakuwa na
wilaya nne za Makete, Njombe, Ludewa na Wanging’ombe wakati mkoa wa
Simiyu utakuwa na wilaya tano za Bariadi, Busega, Maswa, Meatu na
Itilima.

Makao makuu ya wilaya mpya zilizoanzishwa ni kama ifuatavyo: Buhigwe

(Buhigwe); Busega (Nyashimo); Butiama (Butiama); Chemba (Chemba);
Gairo (Gairo); Ikungi (Ikungi) Itilima (Lagangabilili); Kakonko
(Kakonko); Kalambo (Matai) na Kaliua (Kaliua).

Nyingine ni Kyerwa (Rubwera); Mbogwe (Mbogwe); Mkalama (Nduguti);

Mlele (Inyonga); Momba (Chitete); Nyang’hwale (Kharumwa); Nyasa
(Mbamba Bay); Uvinza (Lugufu) na Igwachanya (Wanging’ombe).

Julai 2010, kabla Rais Kikwete hajatoa hotuba ya kulivunja Bunge,

Serikali ilitoa uamuzi wa kuunda mikoa mipya minne na wilaya mpya 21.
Hata hivyo, baada ya kuhakiki mipaka ya maeneo hayo yote na kuandaa
maelezo ya mipaka hiyo vizuri (boundary descriptions),wilaya
zilipunguzwa na kubakia 19.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
ALHAMISI, MACHI 8, 2012.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.