Mtangazaji akiwajibika ndani ya Morning Star Radio
Yusufu Mcharia mmoja wa watangazaji wa Morning Star Radio 105.3 fmSasa unaweza kusikiliza matangazo ya Morning Star Radio 105.3 kwa lugha ya kiswahili kupitia satelite katika Hope Channel International,ili kuyapata matangazo yetu inakupasa uwe na Satelite Dish na kulitune katika C-BAND na kuingia katika Satelite ya THAIKOM ndipo utaweza kuipata Hope Channel na utaingia katika channel namba nne ya audio ndipo utaipa Morning Star Radio inayomilikiwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania ikirusha matangazo yake toka Mikocheni B jijini Dar es salaam





10 comments:
Je, Radio yenu haipatikani Mtandaoni? Sisi tulioko nje ya Tanzania wengi tunatumia kusikiliza redio kupitia mitandaoni tu.
Hatutumii "dishes", zinachafua sura za majengo. Katika nchi zisizokuwa na "Cable Channels" ndiko wanakotumia zaidi dishes, mostly nchi maskini.
Radio Maria Tanzania, tunaipata vizuri sana kupitia mtandaoni. Tungependa na ninyi tuwapate.
Mr. MHOJA
Changamkeni hapo mikocheni, maendeleo ni mtandao zaidi sio dish, wekeni vipindi live kwenye net.
kwakifupi wasabato tumezubaa, tulipaswa hata kuwa na mikataba na startimes ili hope ionekane kitaifa kupitia tbc/startimes.
muda ndio huu kabla wapinzani wetu hawajatufungia milango na madirisha.
Tunahitaji pia nyimbo za zamani za kwaya kama vile kurasini na zingine nyingi,tudownload and then injili isonge mbele
BRO EMMANUEL TANG'ALE
JAMANI EBU WAADVENTISTA WOTE TUAMKE HII RADIO SIO ISIKIKE DAR TU EBU TUFANYE MAPINDUZI MAKUBWA ILI ISIKIKE TANZANIA NZIMA NA NJE YA NCHI KWA NJIA YA INTERNET KWANI NI RADIO AMBAYO IMEPANGILIWA VIPINDI VYAKE LAKINI TUNAZIDIWA NA VIKANISA VIDOGO SANA SIE TUKO PALEPALE JAMANI KUMEKUCHA TUFANYE KAZI.
thnx morning star radio! kwa kazi mnayoifanya nzuri!
bwana yesu asifiwe
naomba sana mwongozo wa kujifunza biblia uwabadilishe mwenyekiti DJ maregesi na elizabeth Nyang'ura sababu wanakwaza sio katika radio lakini wanasabaisha roho kupotea
Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya ya injili, kwani ni watu wengi sana wamekutana na Yesu kupitia huduma yenu nzuri.
Nimekutana na shuhuda nyingi sana za watu wanaoingia kanisani si kwa injili nyingine bali kupitia vipindi vya radio hii.
Mungu mnayemtumikia hatanyamaza kimya kama mkiendelea kuwa waaminifu kwake na kuishi sawasawa na neno lake.
Nyagabona D Ngalya
BWANA YESU ASIFIWE SANA KWANI SASA RADIO YETU YA MORNING STAR INASIKIKA TARIME;TUNAENDELEA KUFURAHIA MATANGAZO;MATANGAZO YATOLEWE MAKANISANI ILI WATU WAWE NA TAARIFA: WENU KTK BWANA KENEDY SIMION WERE
Bwana Yesu asifiwe
Kwakweli mimi na familia yangu tunabalikiwa sana na vipindi vya redio morning star hasa lulu za injili na vipindi vya mahubili jinsi mnavyofungua ukweli bila kuficha, Mungu awabaliki na neema ya bwana wetu Yesu kristo iwe pamoja nanyi nyote..
Mimi nawapongeza sana kwa Kazi kubwa na Ngumu mnayoendelea kuifanya MUNGU na awabariki na Awapatie maarifa zaidi na zaidi kundeleza mbali Duniani kote Kwa Neema yake Ushauri wangu sisi Washiriki tunayo nafasi ya kusapoti kwa kadri tuwezavyo mawazo na michango yetu ya hali na mali ili injiri izidi kusonga mbele Bwana Na awabariki sna wote Mtakao soma huu ujumbe.
Post a Comment