Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi imeeleza kuwa waombaji wote walioomba nafasi za kazi / ajira ya Ualimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambao majina yao yametangazwa katika tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi naOfisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI, Wanatakiwa kuripoti tarehe 01 Februari 2012 kwenye Ofisi zaWakurugenzi wa Halmashauri husika kwa ajili ya kupangiwa Vituo vya kazi. Kila mwalimu anatakiwa kwenda kwenye Halmashauri alikopangwa, kwa sababu HAKUNA MABADILIKO
YATAKAYOFANYWA. Ambaye hataripoti ifikapo tarehe 14 Februari 2012 atapoteza nafasi hiyo.
YATAKAYOFANYWA. Ambaye hataripoti ifikapo tarehe 14 Februari 2012 atapoteza nafasi hiyo.





12 comments:
ila majina ya waliyomaliza shahada ndo hayo au yatatoka mengine
HII HAIJATULIA,INAPELEKA WATU PORI
Hizi ni ajira za mwaka jana 2012 si za mwaka 2013
Ajira ziko wapi jaman mbona kauli ya rais hajatekelezwa!
Jaman tumechoka kukaa home .rais ahad yako iko wap jaman ujui kila ahad n yeny kuulzwa cku ya kiama?
mbona hazionekani
NAUMIA KUSOTA NA MTAA HADI SASA,CHAAJABU NDEV NDO ZNAZD JAMAN AIBU KTK FAMILIA TOKEA DRS LA 7 NATEGEMEA NYUMBANI SIO SR WAMENCHOKA JAPOKUWA HAWASEMI.NAOMBA SERKAL IFANYE HMA KTK AJRA ZA UALMU.
Kwani jamani mmesahau kuwa watanzania ni kama watoto wadogo?ambao mkidanganya hata kwa pipi mnatulia???
Inaumiza sana aisee!
Tukisema tz kchwa cha mwendawazimu mnabisha,oooh ajira za walimu ni mwez wa kwanza,sasa mpaka mwez wa pili huu hakuna kitu,cjajua kwann mliamua kutoa ahad za uongo kiasi hyo.
Ni kheri mkasema kweli ni lini mtatoa ajira ili tujue cha kufanya.
Hata kama tunapelekwa bush poa lakini tunaomba waziri yote uliyoyatamka leo mbele ya vyombo vya habari tukifika halmashauri tuyakute ikiwa ni pamoja na kupewa fungu lote la posho ya kujikimu kwa sku 7 na sio mambo ya ya kuanza kuangaishana huko Halmashauri CHONDE CHONDE Wakrugenz maana hawa ndo wamekuwa chanzo cha migogoro kwa WALIMU wapya.AMINA!
Post a Comment